21 Mar 2023 / 108 views
Rashford, Mount na Pope waachwa England

Mshambuliaji wa Manchester United, Marcus Rashford, kiungo wa Chelsea, Mason Mount na golikipa wa Newcastle United, Nick Pope wameachwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya England kutokana na kukabiliwa na majeruhi.

Rashford alipata majeraha kwenye mchezo wa robo fainali ya kombe la FA dhidi ya Fulham ambapo Manchester United walishinda 3-1 na kutinga nusu fainali.

Pope ambaye amecheza mechi 10 kwenye kikosi cha England alipata majeruhi kwenye mechi ya ligi kuu soka nchini England dhidi ya Nottingham Forest ambapo walishinda 2-1.

Pia Mount anaendelea kupona majeraha yake kwa hiyo ataendeea kusalia Chelsea kwa ajili ya kuuguza jeraha lake hilo.

Kocha wa England, Gareth Southgate alimjumlisha mchezaji huyo kwenye kikosi chake lakini kocha wa Chelsea, Graham Potter amesema baada matokeo ya vipimo vya afya vinasema kuwa hawezi kujiunga na timu ya taifa.

Mount hakuichezea Chelsea toka mwezi wa pili kwasababu ya majeraha ya mifupa yalikuwa yanamsumbua mchezaji huyo na kukosa mechi ya Jumamosi iliyopita dhidi ya Everton.

Rashford amekuwa na kiwango cha hali ya juu kwa Manchester United msimu huu ambapo ameshinda jumla ya magoli 27 kujumlisha magoli 19 aliyofunga baada ya kumalizika kwa kombe la dunia.

Golikipa wa Tottenham, Fraser Forster mwenye umri wa miaka 35 ameitwa kwenye kikosi cha England akichukia nafasi ya Pope.

England watacheza dhidi ya Italia Machi 23 kabla ya kuwakaribisha Ukrane kwenye mechi itakayofanyika katika uwanja wa Wemble Machi 26 mwaka huu.